The House of Favourite Newspapers

Rais Paul Kagame Ahitimisha Ziara yake ya Kikazi ya Siku Mbili Nchini Tanzania

0

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini Rwanda.

Mheshimiwa Kagame ameagwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye aliambatana na; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

Viongozi wengine waandamizi wa Serikali waliomsindikiza ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.

Akiwa nchini Rais Kagame pamoja na mweyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan walikubaliana kuimarisha masuala mbalimbali ya ushirikiano hususan biashara, miundombinu ya bandari, mradi wa umeme wa Rusumo pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.

MWAKA MMOJA wa FILAMU ya THE ROYAL TOUR: DK ABBAS ANAELEZA ZA NDANI KILICHOPATIKANA…

Leave A Reply