The House of Favourite Newspapers

Rais Putin Aapa Kuendelea Kuimarisha Uhusiano na Korea ya Kaskazini

0
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un (kushoto) akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

RAIS wa Urusi Vladimir Putin ameapa kuwa serikali yake itaendelea kuimarisha uhusiano wake na taifa la Korea ya kaskazini linaoongozwa na Kim Jong Un, katika barua iliyotumwa kwa Kim siku ya ukombozi wa Pyongyang, Putin alisema hatua hiyo itakuwa kwa maslahi ya nchi zote mbili.

Kwa upande wake, Kim alisema urafiki kati ya mataifa yote mawili ulianza katika vita vya pili vya Dunia na ushindi dhidi ya Japan aliongeza kuwa “uhusiano wao wa kirafiki” utaimarika zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini KCNA, Putin alisema uhusiano huo ulioimarishwa “utaendana na maslahi ya nchi hizo mbili.”

Katika barua yake, Kim alisema urafiki wa Russia na Korea Kaskazini “ulioanzishwa katika vita dhidi ya Japan”  “umeimarishwa na kuendelezwa karne baada ya karne”.

“ushirikiano wa kimkakati na wa kimbinu, uungaji mkono na mshikamano” kati ya nchi hizo mbili “umepewa kipaumbele zaidi, katika ajili ya kukatisha tamaa tishio la kijeshi la vikosi vya uhasama na uchochezi” imesema taarifa hiyo.

Umoja wa Kisovyeti ulikuwa mshirika mkuu wa Korea Kaskazini, ukitoa ushirikiano wa kiuchumi, mabadilishano ya kitamaduni na misaada.

 

Leave A Reply