Rais Putin: Kipaumbele cha Urusi Kwa Sasa ni Kudumisha Uhusiano zaidi na Nchi za Afrika
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kipaumbele cha Urusi kwa sasa ni kudumisha uhusiano zaidi na Nchi za Barani Afrika wakati huu ambapo Urusi inatafuta Washirika wapya kukabiliana na vikwazo vya kimataifa juu ya vita ya Ukraine na Urusi.
Putin amesema hayo jana Jumatatu kupitia hotuba yake kwenye mkutano kati ya Urusi na Wajumbe kutoka Nchi za Afrika ambapo amesema Urusi inapanga kuongeza ushirikiano na Nchi za Afrika katika nyanja za nishati, matibabu na usambazaji wa dawa na pia kuongeza idadi ya Wanafunzi wa kutokea Afrika katika Vyuo Vikuu vya Urusi.
Katika mkutano huo uliodhuriwa na zaidi ya Wajumbe 40 kutoka Afrika, Putin amesisitiza kuwa Urusi imedhamiria kuendelea kujenga ushirikiano kamili wa kimkakati na Nchi za Afrika na kuunda ajenda za Kimataifa kwa pamoja.
Mkutano ujao wa Urusi na Afrika, unatarajiwa kufanyika July 26-29 mwaka huu Jijini St. Petersburg nchini Urusi ambapo Rais Putin amesema atauandaa vizuri mkutano huo na kuwaalika Viongozi wa Afrika na Mashirika ya Kikanda kushiriki.
MAANDAMANO KENYA: RAIS RUTO ATOA TAMKO ZITO – “HAKUNA MTU ALIYE JUU ya SHERIA” AMJIBU RAILA ODINGA..
https://youtu.be/t8ZUpoIZNJE