Rais Putin na Waziri Mkuu wa India Waadhimia Kumaliza Vita Dhidi ya Ukraine
RAIS wa Urusi Vladimir Putin amemuahidi Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kuwa anatambua wasiwasi wake juu ya vita inayoendelea kati ya nchi yake na Ukraine lakini amemhakikishia kuwa adhma ya Urusi ni kuhakikisha vita hiyo inamalizika mara moja.
Putin ameyasema hayo katika mazungumzo maalum na Waziri Mkuu huyo wa India huku akimtupia lawama Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuwa ndiye anayetia kikwazo katika kurahisisha mazungumzo ya amani.
Siku ya Ijumaa Waziri Mkuu wa India alimuambia Rais Putin:
“Natambua zama hizi siyo zama za vita, na nimekwisha ongea na wewe kupitia njia ya simu kuhusu suala hili. Alisema Demokrasia, Diplomasia pamoja na mazungumzo ndiyo yamefanya dunia imekuwa pamoja hadi sasa.” alisema Modi.
Ingawa kwa upande wake Rais Putin amenukuliwa akisema kuwa Kyiv imekataa mazungumzo ya amani na kubainisha kuwa ushindi wao utapatikana katika uwanja wa medani.
“Tutafanya kila liwezekanalo tumalize vita hii mara moja, ingawa kwa bahati mbaya wapinzani wetu uongozi wa Ukraine umetangaza kugomea mchakato wa kutafuta suluhu na kubainisha adhma ya kujipatia ushindi wake kupitia uwan ja wa medani.” alisema Rais Putin
Hadi sasa Urusi inatawala sehemu kadhaa za Ukraine ambazo imezishikilia tangu ilipovamia katika nchi hiyo kwa mara ya kwanza Februari mwaka huu.