Rais Ruto Aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Usambazaji Taifa Gesi Mombasa
Leo Februari 24, 2023 Rais wa Jamuhuri ya Kenya Dk William Ruto amezindua ujenzi wa Kiwanda cha usambazaji wa gesi cha Taifa Gas kinachojengwa na muwekezaji mtanzania Rostam Aziz maeneo ya Dongo kundu, Mombasa Kenya.
Akizungumza katika uzinduzi hafla ya hiyo mwenyekiti wa kampuni ya Taifa Gas Rostam Aziz amesema kuwa kiwanda hiko kinagharimu dola za kimarekani zaidi ya milioni 200 na kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi gesi tani elf 45 ambapo mradi utakamilika ndani ya miezi 15.
Kwa upande wake Rais wa Jamuhuri ya Kenya Dkt William Ruto amempongeza muwekezaji huyo na kumuagiza kwa Dkt Samia suluhu Hassan Rais wa Tanzania kumwambia kuwa Kenya iko tayari kwa uwekezaji kutoka Tanzania kwani sio lazima muwekezaji atoke maeneo ya mbali kama uingereza na kwingineko hata Africa wanaweza kuwekeza Kenya