The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aanza Ziara Rasmi ya Kiserikali Nchini Msumbiji leo – Picha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi wakati walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara yake Rasmi ya Kiserikali nchini humo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 21, 2022 ameanza ziara Rasmi ya Kiserikali nchini Msumbiji

Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Ikulu ya Maputo.
Rais Samia  akisalimiana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi kabla ya kuanza mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Ikulu ya Maputo leo tarehe 21 Septemba, 2022.
Rais Samia akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi wakati wakiangalia Gwaride la Heshima likitoka kwenye Viwanja vya Ikulu ya Maputo nchini humo.
Rais Samia akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Maputo.
Rais Samia akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa kwenye mapokezi rasmi yaliyofanyika katika Ikulu ya Maputo nchini humo tarehe 21 Septemba, 2022.
Leave A Reply