The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Ikulu Chamwino Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifanya  Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) Bi. Catherine Russell, leo tarehe 11 Machi, 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) Bi. Catherine Russell, leo tarehe 11 Machi, 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia ameishukuru UNICEF kwa mchango wake katika masuala mbalimbali ikiwemo afya, elimu na lishe kwa watoto pamoja na afya ya msingi.