Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa IMF

Rais Samia SuluhuHassan, leo amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Fedha Duniani (IMF), Kristalina Georgieva kuhusu ushirikiano kati yaTanzania na IMF katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

 

Rais Samiaamemueleza mkurugenzi huyo juu ya hali ya uchumi wa Tanzania kwa sasa ambapoukuaji wake umeshuka kutoka wastani wa asilimia 6.9 mwaka jana hadi asilimia 4.7 kutokana na changamoto za Janga la Corona na kwamba Tanzania inahitajikushirikiana na IMF katika kunusuru sekta zilizoathirika zaidi.

 

Mkurugenzi huyoamesema IMF ipo tayari kutoa ufadhili wa haraka kwa Tanzania katika sektazilizoathirika zaidi na kueleza kwamba IMF imepanga kutumia dola za Kimarekani650 kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ili kukabiliana na madhara ya Corona.
Tecno


Toa comment