The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron – Video

Rais Samia akiwasili katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya Mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Nchi hiyo Emmanuel Macron tarehe 14 Mei, 2024
Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais Samia  akiongoza ujumbe wake katika mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Paris.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024. Wa kwanza Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo ya Kitaifa ya Ufaransa Dkt. Chrysoula Zacharopoulou wakiwa wameshika Tamko la Paris katika kuimarisha ushirikiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kikao pamoja na Viongozi mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia na Mwenyeji wao Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa Mei 14, 2024.