The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Viongozi Mbalimbali – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ambapo kwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka kama ifatavyo:-

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Ally Possi kuwa Wakili Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Boniphace Luhende.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Possi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

Profesa Palamagamba Kabudi amerejeshwa kwenye nafasi ya Waziri wa Katiba na Sheria akichukua mikoba ya Dkt. Pindi Chana.
Aliyekuwa Murugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari ameteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali akichukua nafasi ya Dkt. Eliezer Feleshi aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Johari alikuwa miongoni mwa viongozi waandamizi waliosaidia kutoa ufafanuzi wa kisheria wa baadhi ya vifungu vya mkataba wa uwekezaji wa kampuni ya DP World na Serikali kwenye bandari ya Dar es Salaam vilivyodaiwa kuwa na utata.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Pindi Hazara Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Angellah Jasmine Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.