The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

Dkt. Ismael Aaron Kimirei ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwa kipindi cha pili.

Balozi Ernest Jumbe Mangu – Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kipindi cha pili.

Dkt. Marina Alois Njelekela – Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), akichukua nafasi ya Prof. Charles Mkony aliyemaliza muda wake.

Bw. Juma Hassan Fimbo – Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Prof. James Epiphan Mdoe – Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), akichukua nafasi ya Dkt. Andrew Kitua aliyemaliza muda wake.