The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Watumishi nane Kuwa Mabalozi

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewateua watumishi wafuatao kuwa Mabalozi

i) Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).

ii) Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).

iii) Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.

iv) Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.

v) Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.

vi) Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.

vii) Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba

viii) Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi, Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.

Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.

ALBERT CHALAMILA MKUU MPYA wa MKOA wa DAR AMEPANDA, AKASHUKA, AKAPANDA na SASA AMEPANDA TENA…

Leave A Reply