The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Ziara ya Kihistoria Afrika Kusini Ahimiza Ushirikiano wa Kiusalama na Biashara

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati akizungumza na Wanahabari wakati wa Ziara yake ya Kiserikali Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 16 Machi, 2023.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ziara yake ya kiserikali nchini Afrika Kusini amehimiza ushirikiano zaidi wa kiusalama na biashara kati ya nchi hizo mbili.

Rais Samia amekutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mji mkuu wa Pretoria siku ya Alhamisi ambapo ujumbe wake wa Baraza la Mawaziri ulijadili fursa za biashara na makubaliano yanayowezekana na wenzao wa Afrika Kusini.

Hii ni ziara ya kwanza rasmi ya Rais Samia nchini Afrika Kusini tangu awe rais wa Tanzania kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli mwaka 2021.

“Tumekubaliana kuimarisha ushirikiano wetu katika maeneo ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Afrika Kusini ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Tanzania,” alisema Rais Samia. Aliongeza kuwa utalii na viwanda ni sekta zinazoongoza kwa uwekezaji.

Ramaphosa alisema kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini kinaendelea kuongezeka lakini kinaweza kuboreshwa zaidi.

Rais Samia Suluhu Hassan akivalishwa Nishani ya Heshima kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuzungumza na Wanahabari katika ziara yake ya Kiserikali, Pretoria.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati wakielekea kwenye Viwanja vya mapokezi ya Viongozi vilivyopo katika Ofisi za Majengo ya (Union Buildings), Pretoria.
Rais Samia Suluhu Hassan, akitoa Heshima mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo la Makumbusho la Freedom Park Memorial Museum lililopo Pretoria.

RAIS SAMIA ASHIRIKI JUKWAA la BIASHARA KATIKA ZIARA YAKE ya KISERIKALI – AFRIKA KUSINI…

Leave A Reply