Rais Samia Afuatilia Uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025/26 – Video

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amelitangazia bunge kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa akifuatilia kwa njia ya runinga bajeti kuu ya serikali inayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.