Rais Samia Akutana na Papa Francis Vatican Leo
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Februari 12, 2024 amekutana na Papa Francis Vatican.
Rais Samia pia amekutana na Katibu Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin na viongozi wengine akiwemo Paul Richard Gallagher anayeshughulikia uhusiano wa Vatican na mataifa mbalimbali duniani.