The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ampa Shigongo Bilioni Tatu Za Maendeleo Buchosa -Video

0

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Buchosa.

 

Shigongo ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Nyamagana, katika Mkutano wa Rais Samia na Vijana wa Mwanza kwa niaba ya vijana wa Tanzania na kueleza kuwa wananchi wataendelea kumtii na kumheshimu Rais Samia ili kuhakikisha mipango yake ya kuyabadilisha maisha ya Watanzania hususani vijana inatimia.

“Ndani ya miezi mitatu kwenye jimbo langu nimepata bilioni tatu kwa maendeleo ya wananchi, sasa najiuliza kama nimepata bilioni kazi yetu ni kumzungumzia rais wetu, sauti yake nyororo, vijana nendeni mkamzungumzie Rais“-Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo

Pia amewataka vijana kuyazungumza mambo mazuri anayoyafanya Rais Samia ili kila mwananchi aelewe jinsi Rais Samia anavyofanya kazi kwa bidii.

Leave A Reply