The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amteua Mizengo Pinda Kuwa Mwenyekiti Baraza la Ushauri wa Kilimo na Chakula

0

 

Rais Samia Suluhu Hassan, ameunda Baraza la Kumshauri Rais kuhusu utekelezaji wa masuala ya kilimo na chakula ambapo amemteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuwa mwenyekiti wake.

Uteuzi huo umekuja kufuatia azimio la viongozi wa nchi za Afrika kupitia Mkutano wa Utoshelevu na Ustahimilivu wa Chakula uliofanyika Dakar, Senegal.

Katika mkutano huo, kila nchi iliazimia kuunda baraza la kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula.

Pia Rais Samia amemteua Godfrey Kirenga, Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT na Andrew Masawe, katibu mkuu mstaafu kuwa wajumbe wa baraza hilo.

Pia Rais Samia amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa sekretarieti ya baraza hilo:

1. Dk. Florence Turuka, Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

2. Dk. Jacqueline Mkindi, Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA na

3. Dk. Mwatima Juma, Mwenyekiti wa TOAM.

Leave A Reply