Rais Samia Amteua, Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo, Matinyi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Matinyi anajaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi baada ya Rais Samia kumteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.