The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amteua Mohamed Malick Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Mohamed Malick Salum kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Kabla ya uteuzi huu Bw. Salum alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Uchukuzi.

Bw. Salum anachukua nafasi ya Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Uteuzi huu unaanza tarehe 14 Novemba, 2023.

Leave A Reply