The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amuonya Waziri Mchengerwa Kusimamia Mapato ya Serikali – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 11 Machi, 2025.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuonya Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa na kumwambia kama hatawachukulia hatua viongozi wa chini yake wanaoshindwa kusimamia mapato ya serikali, atawachukulia hatua viongozi hao pamoja na waziri huyo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 11, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) kilichopo Jijini Dodoma, unapofanyika mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)

Mabanda yaliyokaguliwa na Rais Samia ni pamoja na la Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Benki ya NMB, Benki ya CRDB, Benki ya NBC na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).

Rais Samia akikagua mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 11 Machi, 2025.