Rais Samia Apitisha Panga Tanesco

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme (Tanesco).

 

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Jaffar Haniu  Jumamosi Septemba 25, 2021 imesema pia Rais amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi wa Multichoice Afrika, Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco. “Chande anachukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka.”

Taarifa hiyo pia imemtaja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Kusafisha Mafuta (Tipper), Michael Minja ambaye sasa ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati.

 

“Amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu. Kabla ya uteuzi huu Mramba alikuwa Mshauri Mkuu wa Kiufundi chuo cha ufundi cha Tanesco. “Amemteua Bw. Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA).


Toa comment