Rais Samia Apokea Tuzo Ya Gates Goalkeeper Award, Hyatt Regency – (Picha+Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Akipokea Tuzo ya Gates Goalkeeper Awards Hyatt Regency Hotel Dar es salaam, leo tarehe 04 Februali, 2025.
Rais Samia Suluhu Hassan, amekupokea tuzo ya hiyo ikiwa ni kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana katika uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiwango cha asilimia 80 pamoja na watoto wachanga.
Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu.



