The House of Favourite Newspapers

rais samia asafiri kwenda brazil

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo Novemba 16 kuelekea Rio de Janeiro, Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa kundi la G20.

Rais Samia ameagana na viongozi mbalimbali wa nchi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuelekea Brazil kufuatia mualiko wa rais wa nchi hiyo, Luiz Ińacio Lula da Silva ambapo anatarajiwa kushiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini, kuchochea maendeleo endekevu na matumizi ya nishati mbadala.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali kama vile China, Ufaransa, Argentina, Ujerumani, Italia, Urusi, Korea Kusini, Marenai na nchi nyinginezo na unatarajiwa kufanyika Novemba 18 hadi Novemba 19 mwaka huu katika Ukumbi wa Museum of Modern Art ulioko Rio de Jenairo huku ukiwa ni mkutano wa kwanza utakaohusisha Umoja wa Afrika kama wanachama wake.

Leave A Reply