Rais Samia Ashiriki maadhimisho ya miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi Dodoma (Picha +Video)
Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, na kueleza kuwa amethibitisha kwamba mkutano mkuu haukukosea kumpitisha kwa kura nyingi.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika jijini Dodoma.


