Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Zimbabwe (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe Januari 31, 2025.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
