Rais Samia Atangaza Siku 5 za Maombolezo, Kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati, Malkia Elizabeth II, kilichotokea tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Uskochi.
Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba, 2022 hadi tarehe 14 Septemba, 2022.
Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.
Rais Samia amewaomba watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo.