Rais Samia Ateta na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya – Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya mara baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 09 Machi, 2025. Mzee Msuya pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwanga.
