The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ateua Tena, Ampeleka Mchechu Hazina, Hamad Apelekwa NHC

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Kyando Mchechu kuwa Msajili wa Hazina kabla ya uteuzi huo alikuwa mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Tifa NHC, Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia Rais Samia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurungenzi Mkuu wa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kabla ya Uteuzi huo Abdallah alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya ya Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

Aidha Rais Samia amemteua Mussa Mohammed Makame kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kabla ya uteuzi huoa Makame alikuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi (TPDC) na pia mshauri Mwekezaji wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania, Makama anachukuwa nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu ni kuanzia leo Februari 24, 2023.

 

Leave A Reply