Rais Samia Atikisa Dodoma: Wananchi Wafurika Barabarani Kushuhudia Tuzo Yake! – Video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Februali 4, 2025 amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akiwa na Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award. Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Mhe. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.