The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atoa Maagizo Matatu Muhimu kwa Mawaziri Aliowaapisha

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama Ifuatavyo.

 

Amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Awali Mhe Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, aidha Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe.Balozi Liberata Mulamula.

 

Amemteua Mhe.Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Awali Mhe.Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kutoka kushoto ni Waziri Dkt. Stergomena Tax, Waziri Innocent Bashungwa pamoja na Angellah Kairuki

Amemteua Angella Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

 

Mara baada ya kuwaapisha Mawaziri hao Rais Samia ametoa maagizo matatu muhimu kwa Mawaziri hao ikiwemo Kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutambua mipaka yao lakini pia kuwa na siri.

Leave A Reply