The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atoa Pole Kufuatia Ajali ya Ndege Iliyotokea Ziwa Victoria

0
                                      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa watu walioathirika kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Precision katika Ziwa Victoria leo Novemba 6, 2022.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter Rais Samia ameandika “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya ndege ya Shirika la Precision katika Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Natuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hii. Tuendelee kuwa watulivu wakati huu zoezi la uokoaji likiendelea huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atusaidie.

Leave A Reply