The House of Favourite Newspapers

ads

Rais Samia Atoa Salamu za Pole Kufuatia Kifo cha Mwanasiasa Mkongwe Mrema

0
                                   Marehemu Augustino Mrema  enzi za uhai wake

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe Augustino Mrema ambaye amefariki asubuhi ya leo Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais Samia amesema atamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Agustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema” Amina

Leave A Reply