Rais Samia Atuma Salamu za Pole Kifo Cha Ndugulile
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Rais Samia Suluhu Hassan kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, ametuma salamu za pole.
Ameandika:
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024.
Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.