The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Rais wa UAE

0
Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Khalifa Bin Zayed Al Nahyan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suuhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa falme hizo Khalifa Bin Zayed Al Nahyan.

 

Rais Samia amendika ujumbe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram uliosomeka:

 

“Ni kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kifo cha Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu na kiongozi wa Abu Dhabi, Tafadhari Sheikh @MohamedBinZayed, Familia ya kifalme na watu wa Umoja wa Falme za Kiarabu pokeeni salamu zetu za rambirambi. Alikuwa kiongozi mzuri!”

 

Taarifa za kifo cha Bin Zayed zimeibuka leo ambapo chanzo cha kifo chake ni maradhi ya muda mrefu ya kupooza aliyoyapata tangu mwaka 2014 yaliyomfanya awe mbali na macho ya watu, amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

 

Sambamba na salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Samia mataifa mengine pia yametuma salamu za rambirambi yakiongozwa na mataifa ya Misri, Bahrain pamoja na Iraq.

Bin Zayed amekuwa akionekana kwa nadra tangu augue ugonjwa wa kupooza mwaka 2014

Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani Antony Blinken ametuma salamu za rambirambi akimtaja hayati Bin Zayed kama rafiki wa kweli wa Marekani.

 

Tayari Wizara inayohusika na masuala ya rais imetangaza kuwa kutakuwa na siku 40 za maombolezo ambapo bendera zitapepea kwa nusu mlingoti sanjari na kufungwa kwa ofisi za wizara zote pamoja na taasisi za kiserikali kuanzia ngazi za juu, ngazi za chini pamoja na sekta binafsi kwa muda wa siku tatu.

Leave A Reply