The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Chamwino, Dodoma

0
Rais Samia akimuapisha Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- (Mipango na Uwekezaji) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Juni, 2024.
Rais Samia akimuapisha Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

 

Rais Samia akiwaapisha Bi. Felister Peter Mdemu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum (anayeshughulikia Masuala ya Jinsia na Wanawake).
Rais Samia akimuapisha Zuhura Yunus Abdallah kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambapo kabla ya uteuzi huo Zuhura alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU, hafla ya uapisho imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo June 13, 2024.
Rais Samia akiwaapisha jaji wa Mahakama Kuu, Projestus Rweyongeza Kahyoza.

 

Rais Samia amemuapisha pia Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na amemuapisha pia Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- (Mipango na Uwekezaji), wengine walioapishwa ni Felister Peter Mdemu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum (anayeshughulikia Masuala ya Jinsia na Wanawake).

Rais amewaapisha pia Manaibu Katibu Watendaji wa Tume ya Mipango na Uwekezaji ambao ni Dkt. Mursali Ally Milanzi, Lorah Basolile Madete na Dkt. Linda Margaret Kokulamula Ezekiel, pia amewaapisha Majaji wa Mahakama Kuu, ambao ni Projestus Rweyongeza Kahyoza, Mariam Mchomba Omary, Nehemia Ernest Mandia kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Leave A Reply