The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awaasa Wanawake Kutotelekeza Watoto, Atoa Maagizo kwa RC Makalla

0
Rais Samia amehudhuria maadhimisho ya 25 ya mfuko wa fursa sawa kwa wote

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hssan ametoa rai kwa kina mama kutotelekeza watoto wao licha ya changamoto za ugumu wa maisha wanazopitia.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Juni 27, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC ambapo amehudhuria Maadhimisho ya 25 ya mfuko wa fursa sawa kwa wote ambao umehudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali wengi wao wakiwa ni wanawake na vijana.

 

“Twende tukatoe huduma kwa watoto, tuelimishane wazazi kutotelekeza watoto kama mzazi hawezi kulea mototo pa kumpeleka papo kuna vituo vya kupeleka apelike kuliko kumtelekeza na akakua na baadaye tukawa na Taifa ambalo halina watu madhubuti.”

Wahudhuriaji wa maadhimisho ya 25 ya mfuko wa fursa sawa kwa wote

Kwa upande mwingine Rais Samia amewapongeza Wajasiriamali wadogo wanaofanya kazi ya kuandaa vyakula lishe kwa ajili ya watoto pamoja na bidhaa nyingine lakini pia amewaasa kina mama wasiishie tu kufanya mambo kinadharia badala yake waende wakatoe elimu kwa kina mama juu ya malezi ya watoto wao.

 

Aidha, Rais Samia amewaasa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Uviko-19 ikiwa ni sambamba na kuchanja kwani chanjo bado zipo.

Rais Samia amemuagiza RC Makalla kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha biashara kwa wanawake

Wakati huohuo Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kuandaa eneo maalum kwa ajili ya kufungua kituo cha biashara kwa ajili ya wanawake.

 

Rais Samia amehimiza watanzania kujiandaa na zoezi la kuhesabiwa (Sensa) ifikapo mwezi wa nane ili kuisaidia Serikali kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Leave A Reply