Rais Samia Awasili Ziarani Kenya (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 4, 2021 amewasili nchini Kenya ambako anafanya ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta.

Akiwa nchini Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Kenyatta na kisha atalihutubia Bunge la nchi hiyo litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

 

Aidha, atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya utakaofanyika jijini Nairobi.Tecno


Toa comment