The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awateua Lukuvi, Prof. Kabudi Baraza la Mawaziri

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ambapo kwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Lukuvi anachukua nafasi ya Jenista Joackim Mhagama ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya.

Rais Samia amemteua Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utali.