Rais Samia: Chama cha Mapinduzi Kimeleta Mabadiliko Makubwa Ndani ya Taifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan leo Septemba 28, 2024 ameongea na Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa katika Ukumbi wa Kanisa la Katoliki Bombambili Songea Mkoani Ruvuma, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeleta mabadiliko makubwa ndani ya taifa na mpaka sasa bado hakuna chama mbadala wa kuongoza nchi hii.
Pia ameiambia hiyo kutosita kusimama na kujibu shutuma na mashambulizi yanayotolewa dhidi yake.
“Niwahakikishie ndugu zangu wa UWT, mabadiliko yote yanayotokea ni kwa sababu ya kukiimarisha chama chetu, tukitambua kwamba bado hatujapata mbadala wa chama cha kuongoza nchi hii, kwa hiyo ni lazima tuimarike na tusimame imara kuiendesha Tanzania ambayo tumeifungua kwa fursa nyingi sana.” – Rais Samia Suluhu kwenye Baraza la UWT Taifa, Ruvuma – Rais Samia Suluhu kwenye Baraza la UWT Taifa, Ruvuma