The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kuanza Ziara Ya Kikazi Mkoani Arusha leo Novemba 27, 2024

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya Kikazi Mkoani Arusha Novemba 27, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine atatunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli tarehe 28 Novemba 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda Leo Novemba 26, 2024 amewaambia wakazi wa Arusha kuwa Rais Samia pia atakuwa mwenyeji wa Marais wengine saba wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kuundwa kwa Jumuiya hiyo ya Kikanda.

SPIKA TULIA AZUNGUMZA KIFO CHA NDUGULILE – ”NAFASI YAKE BADO HAKUITUMIKIA – POLENI SANA KIGAMBONI”

Leave A Reply