testiingg
The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kufanya Ziara Mwanza

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku moja ya kikazi Novemba 18, mwaka huu kwa lengo la kuhudhuria maazimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Hospitali ya Bugando.

 

Akizungumza na Global Publishers, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Robert Gabriel amesema “Mhe. Rais Samia atakua na ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakuja kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando”.

“Mhe. Rais anatarajia kuwasili majira ya saa 12 Asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kutokana na hali hiyo ninawaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza wajitokeze kumkali pembezoni mwa barabara mpaka atakapofika Rais wetu,” amesema Eng. Gabriel.

Hospitali ya kanda ya Bugando imebobea kutoa huduma bora za kibingwa na za kisasa ambapo hospitali hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa kutoa huduma za kiafya kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na hata nje ya nchi.

 

Na Johnson James – GPL

Leave A Reply