Rais Samia: Taifa Lazima Lijipangie Mpango Wa Maendeleo, Ukishindwa Kujipanga, Utapangiwa (Picha +Video)

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema ni lazima Taifa lijipangie mpango maalum wa maendeleo kwa sababu ukishindwa kujipanga, utapangiwa kwa masharti magumu.
Rais Samia ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na uzinduzi wa mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.






