The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Meya wa Dallas Kuanzisha Safari za Ndege Kutoka Marekani Mpaka Tanzania -Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongea na Wananchi Uwanja wa Ndege wa KIA akitokea Marekani.

Rais Samia leo Aprili 28, 2022 akiwa Uwanja wa Ndege wa KIA akitokea Marekani amesema Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani, Eric Johnson, anajipanga kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dallas mpaka Tanzania, hiii ni baada ya kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Tanzania waliomuwakilisha Rais Samia ambapo wamekubaliana kuanzisha uhusiano wa kibiashara wa utalii na mawasiliano na Tanzania.

 

“Tukiwa Marekani kuna kundi lilienda kufanya mazungumzo na Meya wa Dallas (Eric Johnson) na matokeo ya mkutano ule kwamba wenzetu wa Dallas wamekubali na wana hamu wafanye Udugu na Miji yetu ya Tanzania, DSM, Dodoma, Arusha na Miji mingine na tunaangalia uwezekano wa kuwa na Ndege zitakazotoka moja kwa moja kutoka Dallas hadi Tanzania, hiki ni moja ya mambo mazuri tuliyoyavuna”

 

“Tumefanya mazungumzo na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) nao pia mambo mazuri tumekubaliana vizuri na kuna fedha kama ile tuliyoleta tukaipeleka kujenga vituo vya afya, madarasa na mengine, tunatarajia nyingine inakuja ya aina ile ili iende kwenye maendeleo” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply