Rais Samia Na Nchimbi Kupeperusha Bendera CCM – Video
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Rais Samia alitangaza pendekezo hilo leo, Januari 19, 2025, katika mkutano mkuu maalumu uliofanyika jijini Dodoma.