Kartra

Rais Samia: Sensa ni kwa Watakaolala Tanzania Tu – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani 2022 itahusisha watu watakaolala nchini kuamskia siku yenyewe ya sensa.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne, Septemba 14, 2021 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji na uhamasishaji kuhusu sensa ya mwaka 2022 inayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

 

“Zoezi la #Sensa linahusisha ukusanyaji wa taarifa muhimu kwenye nchi kuhusu idadi ya wananchi, jinsia zao, umri, shughuli zao na makazi yao, mahali alipo na kazi yake. Zoezi hili sio geni kwetu, limekuwepo duniani tangu karne na karne.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa katika Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mpango wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, leo Septemba 14,2021 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

“Zoezi la #Sensa linahusisha watu wote watakaokuwa wamelala ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamkia siku ya #Sensa, hii ndio tabia peke yake ya sensa hii. Kuna umhimu mkubwa wa kuwahamasisha wananchi kujitiokeza katika zoezi hili.

 

“Kuna hoja nimekuwa nikizisikia kwa nini tutumie pesa zetu nyingi kwa ajili ya #Sensa, ni vyema ukawa na taarifa zako kuliko kutumia taarifa za watu wengine, unapotoa taarifa unasema chanzo ni #SensaYaTanzania iliyofanyika mwaka flani. Kuliko kusema chanzo ni taasisi flani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe kuzindua rasmi Mpango wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, leo Septemba 14,2021 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

“Taarifa za #Sensa zinatumiwa pia na taasisi za Kimataifa, taasisi za kiraia, pia wawekezaji hutumia taarifa hizi kuamua ni aina gani ya biashara kuwekeza na wapi, watafiti wa ndani na nje ya nchi hutumia taarifa za sensa kwa ajili ya tafiti mbalimbali.” -Rais Samia Suluhu.

 

“Sensa itaisaidia Serikali kuandaa Sera kwa ajili ya mpango wa maendeleo, kufuatilia na kupima utekelezaji wa sera hiyo. Kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali za Taifa na kupeleka miundombinu ya maendeleo kwa wananchi wetu.

 

“Huwezi kushughulikia tatizo la ajira kama huna taarifa sahihi kuhusu watu wasio na ajira, huwezi kushughulikia suala la wenye uhitaji maalum bila kufahamu taarifa zao na idadi yao,” amesema Rais Samia.

 

🔴#LIVE: RAIS SAMIA AZINDUA MKAKATI wa UELIMISHAJI wa SENSA, ALIKIBA, DIAMOND WAHUDHURIA…


Toa comment