The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Tozo ya Miamala ya Simu Ipo – Video

0

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haikuwa na nia mbaya kuanzisha tozo ya makato ya miamala ya simu kwani lengo lake ni kukusanya fedha ambazo zitakwenda kuboresha miundombinu ya barabara na maji vijijini ili kuondoa changamoto hiyo

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne, Julai 27, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akihutubia baada ya kumaliza kuwaapisha mabalozi 13 aliyowateua hivi karibuni.

 

“Kuhusu suala la miamala ya simu, kutuma na kupokea tulianza mwezi huu wa Julai, lakini kelele zikawa nyingi wananchi wakalalamika na kwa kuwa sisi ni Serikali sikivu tulipokea maoni yao ambayo tumeyakusanya kwa wiki nzima kusikia wanasemaje, na baadaye nikawataka mawaziri wa waweili wa fedha na teknojlojia pamoja na taasisi zao, Julai 29, 2021 tutapokea maoni ya Kamati tuliyoiunda na tutaujulisha Umma tunakwendaje kwenye hili.

 

Makato ya miamala ya simu tuliyaweka kwa nia njema, wananchi wetu wanalima mazao vizuri tu lakini wakivuna wanashindwa kutoa mazao yaliko kuleta maeneo ya masoko, tatizo njia za vijijini hakuna, sehemu kubwa ya pesa hii itakwenda kujenga barabara za vijijini ili wasafirishe mazao yao yasiwaozee.

 

“Kila mmoja anakotoka kuna shida ya maji, tumefanya asilimia 74 bado asilimia 26, pesa hizi (tozo za miamala) zitakwenda kwenye maji, niwaambie Watanzania hizi tozo zipo, tumesikia vilio vyao, tutaangalia nia nzuri ya kwenda na hili, ambayo haitaumiza watu, serikali ipate na maewndeleo yaendelee, kazi iendelee.

 

Kuna kilio cha kupanda kwa bei za mbolea sababu viwanda vingi huko duniani vilifungwa sababu ya corona, baadae dunia ikasema lazima tujifunze kuishi na janga hili, ulimwengu wote wamejifunza Magufuli Philosophy, janga lipo lazima tujifunze kuishi nalo,” amesema-Rais Samia Suluhu.

 

Leave A Reply