The House of Favourite Newspapers

Rais Trump Aondoka Ikulu na Mkewe Melania (Picha +Video)

0
Rais Donald Trump akitoa hotuba yake ya mwisho katika Kituo cha Anga cha Andrews akisema ilikuwa ni heshima na fursa kubwa kushika wadhifa huo.

RAIS Donald Trump ameondoka Ikulu ya Marekani leo Januari 20, 2021 akiwa na mkewe saa 2:12 asubuhi (Tanzania ilikuwa saa kumi jioni leo) ambapo alizungumza na waandishi wa habari akisema kuwa rais wa nchi hiyo ilikuwa ni ‘heshima ya maisha’.

 

Akiwa katika kituo cha kijeshi cha Andrews, aliwaambia waandishi wa habari kwamba atarejea ‘kinamna’  na aliwaambia wote waliokuwepo: “Muwe na maisha mema”.

 

Wakiwa eneo la Mar-a-Lago, Trump na familia yake watatazama kuapishwa kwa rais mteule, Joe Biden, akiwa rais wa 46 wa Marekani.

Trump akitoa hutoba yake kituo cha kijeshi cha Andrews mwishoni mwa urais wake leo, Januari 20, 2021. 
Trump na mkewe Melania wakiwasalimia watu waliokuwepo kituo cha Andrews.

Trump na mkewe wakiwasili kituo cha Andrews. 
Ivanka (wa pili kulia) binti wa  Trump akiwa katika hafla ya kuondoka kwa baba yake.

 

Leave A Reply