RAIS TSHISEKEDI AMUOMBA JPM – VIDEO

RAIS Felix Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo {DRC} amemaliza ziara yake ya kitaifa ya siku mbili nchini kwa kumwomba Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ili nchi yake ijiunge na umoja huo.

Akizungumza katika siku yake ya mwisho Tshisekedi alisema:

“Namna nzuri ya kudumisha mahusiano yetu mazuri ni kwa kupitia ujenzi wa miundombinu kwani itasaidia kuongeza wigo wa biashara kati ya nchi ya Tanzania na Congo.  Kwa hiyo, naomba niwataarifu kuwa nchi ya Congo tayari imeshaomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki na bila shaka itakuwa jumuiya bora zaidi.”

 

Alisema ili kufikia ukuaji wa uchumi unaotarajiwa ni lazima pawepo ushirikiano wa kuendeleza miundombinu katika nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na reli, bandari na barabara.

 

“Tumekubaliana pia katika ujenzi wa miundombinu pamoja na kushughulikia changamoto ya vizuizi vya kibiashara. Nashukuru kwa mwaliko katika mkutano wa SADC utakaofanyika baadaye na niko tayari kuja katika mkutano huo kwani SADC ni eneo muhimu la kiuchumi ambapo nchi ya  Congo pia ipo,” alisema Tshisekedi.

 

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA


Loading...

Toa comment