The House of Favourite Newspapers

Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

0

MWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, unatarajiwa kuzikwa tarehe 2 Machi 2024, mjini Unguja.

Ratiba ya mazishi ya marehemu Mwinyi imetangazwa leo tarehe 29 Februari 2024 na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akitangaza kifo chake.

“Kwa niaba ya Serikali ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1, 2024,” amesema Rais Samia na kuongeza:

” Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.”

Rais Mwinyi, amefariki dunia leo Ijumaa tarehe 29 Februari 2024 majira ya saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Leave A Reply