Rais wa Brazil Asambaza Jeshi Kuzuia Vurugu

Rais wa Brazil Michel Temer ameyasambaza majeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia, baada ya waandamanaji kuanza kulichoma moto jengo la serikali na kuharibu mengine.

Maafisa wanasema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kudhibiti mambo, baada ya waandamanaji elfu 35 waliokuwa wakielekea mjini na kuongoza moja kwa moja katika bunge la nchi hiyo na katika makaazi ya Rais.

Wakijaribu kuwatawanya waandamanaji, Polisi wamefyatua mabomu ya machozi katika uwati wa watu. Tuhuma za rushwa zinazomkabili rais wa nchi hiyo ndizo zilizosababisha mchafuko huo wa kisiasa.

Kuna wasiwasi kwamba kusambazwa kwa wanajeshi kudhibiti mambo kunaweza kuchochea zaidi vurugu.

Chanzo: BBC Swahili

 

Loading...

Toa comment